Waks za Prof ninda ya Sheng

October 21 2014 10:15am     0 671

Photo Credit:Google   Tingua risto

Angalau Prof Ali Mazrui aliweza kupumzika fiti baada ya kuzikwa hasapo haribu na Fort Jesus, Sunday 19th Oct 2014. Mazrui aligenya akiwa Oteto na ilibidi mwili yake kurudi mtaani Old Town, Coasto,  ndio afanyiwe maombi na kukuwa laid to rest.

Tungependa sana kumbuka vipoa kupitia waks zake kama Scholar jamo mnoma vimost. Aliweza kuchora mbuku kibao na ata pia alishugulisha na kutambuana na lugha ya Sheng. Kama Prof ungedhani angekuwa msee wa fao kudiss Sheng, lakini badala yake aliweza kuiembrace. Alisaidia wadhii wengine kama; Nathan Oyori Ogechi na Mokaya Bosire, kufanya research na kuandika kuhusu hii lugha wasee wengi hudharau.

Alikuwa ameanza hiyo waks kitambo juu kuna hadi mbuku inatambulika Slang and Code Switching yenye aliandika 1995. Alafu hisihi ndio ilikuwa jamo ya mbuku zilitumiwa kama reference na hao writers wengine.

Enyewe tutahata hiyo mind smata vimost. Sidhani kuna msee anaweza toshea kwa njuta za huyu mjamaa.

 

Related Stories