Gava inadai kuban mtush
Photo Credit:Google Tingua risto
Kuna mraa inaendelea, ikidaishwa gava za East Africa zinapanga kuban mtush. Ambapo watastopisha importation ya cladi na njuta zote za 2nd hand, zinatoka majuu. Na hii riba italeta ngori haijuani kwa hii industry ya mitush.
Venye maprezo walipatana kwa summit ya kinde na six ya East Africa, waliamua itakuwa fiti kuchuja mtush kwa bizna ata ikiwa inaingiza mamilli, eti ndio waweze kuboost local textile na leather industries.
Eti kudiscourage imports za mtush, gava imekuwa ikihike tax za imports. Lakini tangu Uhunye kuingia Orezo, alidundisha izo rates kiasi kutoka $0.30(sh27)per kilo to $ 0.20(sh18)per kilo.
Kumaanisha hizo gava zimekubali hii risto, zitalazimika kumoderate prices za hizi products. Sa blanda itaangukia maasafara wenye wamekuwa wakiweza kuafford cladi za mtush solo. Manze wataumia kama hii mradi itaendelea.