Mambo kadhaa za kutambua…

June 30 2015 4:42pm     0 259

Photo Credit:Google   Tingua risto

Hasapa ni advice zenye zina apply kwa raiya wa mayadi zote. Kuna mambo unafaa tu kuduu bila kuambiwa juu inatambulika kama common courtesy. Enyewe tushawai skia that ni fiti kufanya vitu fiti kwa wasee ndio pia hao wakufanyie the same.

Kuna venye ukaborrow ndae ya beshte, unafaa kurudisha ikiwa full tank, kama njaro ya kusema thanx. Hasapa 254 inaweza kukuwa hard, labda italingana kama bei ya ngata imedunda alafu tunaweza kuskizana kwa hii fact.

Usiwahi vuta fegi kama unacheki wadhii wako karibu na wewe wako uncomfortable. Inakatsia sana kujua ukona deathwish lakini usiingize kila msee kwa hii mpango yako. Manze respect health za wadhii wengine by kukwama kwa smoking zone ziko jiji.

Mabeshte wakimuja kukusaidia na waks za keja, walipe na keroma. Na sio tafadhali bana. Hanaku kitu mbaya kama kuenda kusaidia mudhii kumaha alafu anawaacha mataani. Ata kama utaweza afford sembe na greens,  chipo mwitu ama mandunya na daso, it’s the thought that counts.

Ile muhimu kwa hizi zote, manze ukikopa mkwanja ata ikuwe ni less aje kwa opinion yako, RUDISHA bana. Usidhanie juu msee amekuwai ni kumaanisha hana waks ya hiyo ganji. Ata kama hajakuitisha, haimanishi eti sasa unafaa kukaa na hiyo mkopo foree.

Mambo zingine less kama ukidoze kwa msee, kabla hujaishia, tandika bed ama mekisha hiyo area ikae neat. Ama msee ameamua kukupikia, usitoke kabla hujamsaidia kuweka dishes safi. Alafu msee amekuwai nangos ama lapii yake kuduu kitu, manze uaianze kupitia stuff zake bila kupewa ruhusa. Tena ukiomba mbuku, make sure umeregesha kwa mwenyewe.

Na kwa wale wakona ufala ya kudump msee through SMS, temana na hiyo risto. Kama umekuwa mjamo ya hao wasee huduu hizi stuff, jaribu kuanza kubadilika na utakenga blessings fogo zikimuja your way.

Related Stories