Tafash za mathree!

June 30 2015 5:17pm     0 318

Photo Credit:Google   Tingua risto

Kila mvua lazima kukuwe na ngori nifla kwa matatu industry. Ishakuwa kawa lakini kila time, raiya ndio hukapitia kukiwa na noma kati ya gava na wadhii wa mat. This round kuna threats wamemekisha mapema, wakidaisha watakuwa na strike on weno ya 1st July.

Of late, mathree zimekuwa zikijiingiza kwa aksi zinengi mwenda na kuzidisha hasapa ninda ya jiji. Kitambo tulikuwa tunablame zile huenda long distance, lakini inakaa madere wamekuwa wreckless kuruka. Blanda ni eti wateja wale huwatetea ndio wanaumia nab ado hawataki kukubali responsibility.

Kumekuwa na aksi ambapo mat ya ronga, inengi ya LA, alafu sasa ile recent ikiwa ya Doni zimehusika. Kwanza hisihi ya lachu, ililazimisha National Transport and Safety Authority (NTSA), kuban Embassavo Sacco kutoka kwa baro.

Hisihi sasii imekuwa ikiendelea wiki nzima na haijulikani itakatika lini. Mabuu zinengi zimekuwa zikitry sana kuduu waks hiyo rotejo lakini raiya wamekuwa fogo kuliko mandae za kucommute. Kumaanisha already wadhii wanateseka.

Sa kama bado mat zitastrike, basi kutakuwa noma kufika kwa majanta ama chuo. Alafu hii side inengi Director General Francis Meja wa NTSA, anadaisha mathree zile zitagoma, zikuwe ready kuchujwa kutoka kwa industry, juu hawatabadilisha decision yao.

Related Stories