Kenya kukachora huko Beijing

August 31 2015 10:45am     0 637

Photo Credit:Olympics   Tingua risto

Kama kawa, lazima raiya ya 254 ikiingia kwa masehemu iwakilishe kabisa. Hii haikua any different vile wadhii wa #TeamKenya waliingia Beijing World Athletics Championship za 2015 pale China. Kutoka kwa nduthe, masafa na hata javelin, hawa maboiz na wasupa walikua tu wanakwachu hizi ndechu mbaya mpaka imabaki vile compe zimelandi, Kenya ndio iko pale juu kwa rankings. Hii ni after kushinda country zingine zote noma ka kina Jamaica, Oteto, Brito na hata Ethiopia. Kenya ilipata na Gold saba (7), Silver sita (6) na Bronze tuta (3)

Ugoro zilitoka kwa wasee ka David Rudisha mwenye alikua fao kwa ndudhe za Mens 800m, ingine kutoka kwa Vivian Cheruiyot, msupa mwenye aliponyoka na kua fao kwa Womens 10,000 m (10Km). Sio hao tu kwa kutoka unyoya, kuna bado huyu mzito Ezekiel Kemboi mwenye alikua fao kwa Mens 3,000 m bila kusahau msupa Hyvin Jepkemoi mwenye pia aliponyoka na ugoro ya Womens 3,000 m. Kuna pia huyu mzito, Asbel Kiprop mwenye pia alikwachu ugoro ya Mens 1,500 m na hii ndio ilikua ugoro ya lanyo yenye 254 iliwai kwa hizi compe. Kiprop alidaisha vile alikua amejinice mbaya kua kwa hii rende ya kuwai wins za nguvu hii design.

Msee mwenye pia hawezi sahaulika ni husuyu mzito, Julius Yego mwenye aliwai ugoro kwa javelin. Hii ilikua mara ya fao kwa raiya wa 254 kuwai medal hasapo na pia karibu avunje world record yenye iko saa hii vile alitupa hio brungo distance ya 92.72 m . World record yenyewe saa hii iko at 98.48 m na ilisundwa na Jan Zelezny kitambo kiasi, back in 1996. Kitu mwenda yenye ilifanya raiya ibambike sana kuhusu mzito Yego ni vile alianza kujifunza kutupa hii javelin akitumia Youtube, na sasa amewai ugoro kwa compe za World Championships. Hii ni riba ya aajab jo na hata ka hakuwai hio record, bado kuna day ingine!

Vile compe zililandi na hizi rankings zikatangazwa, msee wa fao kupea hii jeshi conrats ilikua Orezo mwenyewe, Onyato na hii tweet akidaisha vile wasee wamefanya poa sana.

 

Related Stories