Fika chachiko...lakini bila weave!

August 20 2013 5:18pm     1 677

Photo Credit:By Praise Station   Tingua risto

Madem huwakilisha kupitia vile wameng'ara ama vile wamemek nywele. Mapasi nao hucharaza wasee na teachings zao bila kugwaya vile raiya wataichukulia. Wengi wa hawa mapasi ni ka hua wanachukulia hio position ya kua pasi personal, inakua ni ka kupeana personal idea ama kusuka umati kulingana na vitu hao wanataka, sio tu kupeana leadreship ama teachings za mbuku ya Sir G!

Sa kuna pasi mjamo anaitwa A.J Aamir wa chachiko inajulikana kama Resurrecting Faith huko Texas, Oteto. Anadai hapendi madem waking'ara weave. Kwanza ata yeye huwakataza kuzivaa kabisa especially wakikam kwa chachiko yake.

Sababu yake ni ati, madem wanazicladi hawajiamini na wengi wao ata hawawezi afford kuget weave juu itabidi ametumia thao mbao kuanua jamo ya nguvu. Kwake anaona hii ni mkwanja most tu sana kwa wasee wake na ni mkwanja wanaweza tumia kudo vitu zngine instead of kuget mbalas.

Amedai ataendelea kuzua noma hadi mamanzi waache kujilazimisha kung'ara vitu fake na wajiamini juu ni wasupuu design wako bila hizi vitu imbo. Unakubaliana nahusuyu pasi ama kuna vile amevuka mpaka hasapo?

Related Stories