Teaser kwa fans wa GoT

November 24 2015 7:55pm     0 582

Photo Credit:India   Tingua risto

Kuna raiya ilikua imetulia kiasi lakini sasa wako pabaya tena, hii ni rende ya series nifla ya HBO, Game of Thrones. Hii ni series nifla kwa mbulu yenye iko adopted from mbuku za mzae anajiita George RR Martin. Mbuku ya husuyu mzae jamo ndio ilichukuliwa na wadhii kadhaa, wakaamua kuifanya series na saa hii wasee wanangoja Season 6 kwa hizi installments. Story yenyewe kwa hii series iko set time za tene, time za Kingdoms na zile familia zilikua zinatawala hizo enzi, wakipigania power.

Kwa wasee wamekua wakiikenga keenly, Season 5 iliisha place jamo ya ngori sana. Favorite mjamo, Jon Snow (Kit Harrington) alikua amedungwa ukapi kadhaa na mabeshte wake, Brothers of the Night Watch. Hapo hapo wasee walikimbia kwa mbuku kucheki fate ya husuyu character kwa upcoing series lakini bado mbuku haijatoklezea. Theories zimekua kibao kwa mtandao wasee wakisema Jon Snow hawezi dedi ama atafufuliwa na dem flani ako na magical powers. Na isitoshe, HBO wenyewe waliamua kukanyagia hio story kabisa.

From writers, actors na staff wote wako kwa shooting ya hii series, hata Kit Harrington mwenyewe, hanaku msee amefichua ka character ya Jon Snow itakua kwa Season 6, lakini tweet yao ya teaser poster wakiambiana dates za season kuanuliwa ilikua ya kuchocha tu zaidi. Hii iko na mbisha ya Snow na inakaa ako na damu kiasi kwa uso. Wamesunda mpaka date na inakaa wasee watangoja mpaka April 2016 kujua fate ya husuyu mzito, Jon Snow.

Uko kwa rende ya kusema Snow anarudi ama unaona ashadedi kabisa wasee wakubali tu?

Related Stories