Ghana wakakatsia Germany na draw ya 2-2

June 22 2014 9:47am     0 1858

Photo Credit:Getty Images: Martin Rose   Tingua risto

Kuna vile jo, after mraiya ichangamke bila kudoze, Ghana ilipatia Africa yote hopes nira venye walimenyana na Germany huko Brazil kwa stadi ya Fortaleza venye wali endana draw ya 2-2 kwa match yao ya Group G.

Game ilikuwa na ma tension kadhaa kwa first half but hiyo pupa yote haiko toa bao hata jamo. Second-half iliwaka moto after dakika ngovo venye ma Germans walikamua game omole after kuhandwa na Ghana, Mario Gotze alihedi cross mwenda kutoka kwa Thomas Muller.

Wajeru hawakuwa wame malo kunice-ika na bao, waka legea kiasi design waka achia Andre Ayew gap bwaku ya kuhedi ball na dabo goalie wa ujeru Manuel Neuer hakuweza kustopisha.

Haikumalo dakika kinde, wadhi wa Ghana waka changamka venye Sulley Muntari alichenga moja! aka chenga mbili! akapenya midfield akawahi Asamoah Gyan pass yenye aka control kabla aiwange past goalie wa ujeru.

Germany kumbe walikuwa wamefichia Ghana whiteball. Otero wa Germany, Miroslav Klose alitoklezea kwa corner ya goal aka dandia ball ilikuwa loose hapo ndani ya 18.Hiyo bao ilimake Klose apate bao ya 15th kwa World Cup finals play. Sasa ako same level na Ronaldo wa Brazil kama leading scorer. Besides hiyo, sasa yeye pia ndio player wa thadho ku tinga bao kwa tourna nne sama na Pele na Uwe Seeler wa Germany.

After hiyo, match ika baki na manduki na ma pass mwenda ziki happen both sides but hakuna bao ilipatikana. Sasa Germany ina points nne na Ghana wako hai kwa Group G. Teams zote limbi zita get kupumzika siku nne kabla Germany icheze Oteto huko Recife on June 26 na Ghana iende Brasilia kucheza against Portugal.

Related Stories