Naija ika nyamazisha Bosnia and Herzegovina 1-0

June 22 2014 11:32am     0 428

Photo Credit:Getty Images   Tingua risto

After Ghana kucheza match ya pawa against Germany, mabroda wa Naija walikuwa wanajua Africa yote ina wamurika vibaya. Walingia uwanjo na nia jamo ya kumalo Bosnia and Herzegovina bila blanda kama game yao ya fao against Iran yenye walitoka draw bila mabao.

Match ilikuwa huko Cuiaba kwa stadi ya Arena Pantanal na stadi ilikuwa imenasho kuruka.

Bao ya Peter Odemwingie yenye ilitingwa kwa first-half goal iligei maOga points nne kwa Group F kabla wakutane na Argentina wenye wako already kwa knockout stages.

Kuna point flani, bao jamo ya Bosnia-Herzegovina ile canceliwa juu ya offside though ma replay zilishow poa sana Edin Dzeko alibeat goalie wa Naija, Vincent Enyeama vikilin bila shida but ref alikwara.

Madrama hazikustopia hapo juu at the 29th minute, Emmanuel Emenike alitoka chwa side ya right akaskuma Emir Spahic wadhi wa Bosnia-Herzegovina waka dhani amefouliwa but wapi? refa tena aka allow game iendelee aka play advantage ndio Odemwingie aliget hiyo pass aka tinga bao yake.

Bosnia-Herzegovina walikuwa wana ng'ang'ana kusumbua mabroda but mafufu na yam za mabroda ziliprove kuwa asset mwenda juu maplayer wa Bosnia-Herzegovnia walikuwa wana anguka down kama ma nzi.

Mabroda waliweka presha mwenda design karibu Emenike atinge bao inengi but goalie, Asmir Begovic aliiblock kabla Edin Dzeko atry shot jamo ya pawa yenye ili wanga post na kukazia Bosnia-Herzegovina kuwahi bao.

Related Stories