Wyclef Jean Ku collabo na Kaka sunguch

September 18 2014 1:26pm     0 1608

Photo Credit:Starndard Digital   Tingua risto

Wyclef Jean amekuwa 254 kwa masiku kadhaa saa hii, juu ya coke studios projects. Tunatambua Wyclef na mangoma zake noma noma na bado rende yao yenye ilikuwa inajiita the FUGEES, wakiwa kimoja na Pras Micheal na Lauryn Hill. But Jean alichorea hii rende na kuamua kufanya mambo ki man solo.

Ata baada ya kuchorea the Fugees 1997, tunacheki amekuwa akipata ma grammy awards kadhaa akiwa man solo. Akiwa hasapa 254 Wyclef alipata chance ya kumeet wasaani kadhaa pamoja na Budha Blaze mwenye amekuwa akiwakia hii project. Kwa hiyo harakati Budha Blaze alidaisha Wyclef atapata chance ya kuwork na Rabbit aka Kaka Sungura.Na jana usiku tuliconfirm na kaka sunguch baada ya kudaisha anaingia studio time kiasi na Wyclef so wasee wategee.

Ata hivyo jana bado ilikuwa siku bigi sana kwake Wyclef Jean. Alikuwa set kuhave dinner State House na Orezo Uhunye. Juu amekuwa aki participate na mambo ya politics kwa country yake husuko Haiti. Tunakumbuka 2010 alitry kuwai seat ya Orezo but hakufaulu, juu hajapoa Haiti for five years continuous, tunajua amegrowia steto tu.

Na bado Wyclef aliweza meet na Muthoni the Drama Qeen na Blinky Bill so tunategea kuyebi ni nini hawa ma artist watachomoa.

Related Stories