Manze mind jamo mzito imekaukata…

October 14 2014 12:53pm     0 602

Photo Credit:Twitter   Tingua risto

Hii Monday jamo ya October 13th 2014 itabaki kua etched into memory za mtu kibao kwa hii famo yetu ya hasapa 254, and mostly kwa wasee wamegusa mbuku, poems na research za husuyu mzito, Prof Mazrui, ama ukipenda, Prof Ali Al’amin Mazrui. Reason hii day inabaki kua remembered ni juu hii day Prof Mazrui aligenya akiwa hosi nifla huko Oteto after kukua msick for a while.

 

Prof Mazrui ni mzito wa hasapa 254, na alizaliwa side za coasto, 24th Feb 1933. Na amekuwa msomi life yake yote, akiwa amefika chuo za hasapa Kenya na zinengi husuko majuu. Isitoshe akona awards kibao lakini ile bwaku vimost ni kukuwa recognised kama mjamo wa the world’s top 100 Public Intellectual. Sema kukuwa chopi!

 

Prof ni acclaimed writer wa over mbuku salasa, poems over so jamo, na research yake imetumika kwa thesis mob kwa wasomi. Kazi yake yenye hasapa inatugusa sana ni tribute na waks zake around Sheng. Language na culture ya Sheng imepata pang’ang’a most, positive na negative kutoka kwa wasomi alike, lakini Prof Mazrui alikua mjamo wa wale wasee walikua washaiyebi na wameona ni kitu inaenda far, design ya Ngoso na Swa.

 

Waks zake about Sheng ni most online, hatuwezi zichambua zote...but ni blanda vile amekamanyuria. Ata hivyo amekuwa survived na wifey mjamo na waniaju wasita.Tutaendelea na hii task ya ku-preserve & demystify Sheng mzito, may you rest in Peace.

Related Stories