Trend nira hasapa 254

November 17 2014 9:44am     3 1709

Photo Credit:Google   Tingua risto

Ndeima ya 17th Nov 2014, siku imeamuliwa ikuwe ya kamtula na mambuus.  Hasawa ni wenye walikula machungu na majamaa wenye wanaenda wakichujana cladi kwa street eti juu hawajang’ara vipoa.

Kutoka last week, kumekuwa na vurugu sana kuhusu risto nifla yenye ilitokelezea hasapo CBD. Baada ya mbuus mjamo, kuvuliwa cladi juu zilikuwa revealing sana. Zaidi ya  hii noma kutokelezea kwa rotejo, machali ndio walianzisha na wakachukua hadi videsa, yenye imesambaa kwa internet kama hotcake.

Kama bado wasee wanazusha kwa social mediahadi wakaanzisha campaign inajiita #MyDressMyChoice, manzi mwingine alivuliwa tena cladi  na husuko Coasto. Kile inakatsia more, huyo kwanza alikuwa ameng’ara toja. So unaweza shangaa kwani ni cladi gani yenye inafaa sasa.

Alafu hawa majamaa wanafanya hii kitendo wanasaidiaje society? Juu hanaku venye unaweza kuniskiza eti heri mdem kukuwa ndethe kuliko akiwa ameng’ara zile tight ama zile short. Tena ni ufala kuruka, ukikumbuka mababu zetu ata hawakuwa wanacladi any. Kumaanisha tumejaza tu mapervt na wasee wako idle, wakisaka risto za kuchapiana wakiwa base.

Ama ukona maoni gani?

 

Related Stories