Ukumbusho ya Saint mjamo mnoma

March 17 2015 2:51pm     0 1741

Photo Credit:Google   Tingua risto

Kama miaka soh nnei baada ya yesu kuzaliwa, kulitokelezea Priest mjamo alijulikana kama Patrick na alikuwa antambulika sana kwa venye aling’ang’ana kuspread gospel dunia nzima. Lakini kabla kufika hasapo, aliwai kudnapiwa akiwa miaka kinde na six, na Irish Pirate, wenye walimkinda kama slave.

Alibaki husuko Ireland miaka sita, na iilibidi amekaribia Sir God, juu ya venye alikuwa anaomba kila night asevike. Siku jamo aliweza kuhepa, baada ya kuskia sauti ya Angel, na kuget boat ilikuwa inaenda Britain. Alirudi kuenda France kwenye alichop kukuwa priest.

Baada ya kumekiwa Bishop, alirudi Ireland, kujaribu kuconvert hao mapagans. Lakini sana sana alikuwa anadai kuenda kuconvert slave owner wake mwenye alitambulika kama Milchu. Kuna parasha kadhaa zenye hudai Milchu alidhani Patrick anamuja kurevenge, so akajimada.

Patrick alikatsika lakini bado akazidi na kujenga chachiko ya fao na akawa anambetea kila area akipreach kwa raiya hadi Kings na Chieftains wa hizo mayadi. Sa alipata kukuwa na enemies fogo juu walicheki nia kama hiyo Christianity alileta alichanua raiya na bizna yao ya slavery ikawa imespoil.

Wadhii kadhaa walitaka kumdedisha lakini hawakufaulu. Aliendelea wera yake ya chachiko hadi akiwa mzae na akagenya date same na March 17, ndio maana kila mwaka wadhii humkumbuka wakicelebrate St. Patrick’s Day.   

Related Stories