Udingo kwa parking za supa!

August 8 2014 1:33pm     0 1939

Photo Credit: John Bosco Mwaura   Tingua risto

Manze! Kunasemekana raundi hii, udingo imezidi sana kwa ma parking za supa. Unajipatanga ukiwa umetoka janta umekatikiwa na nguvu, saa unadaisha tu kuingia supa dakika kiasi tu ukwachu burungo moja mbili dakika kama kinde na kobole. Kwa ndai saa hizo umesare ma gadgets za koya, kama tenje, laptop, vitu kama hizo na ukatinga mgola za ndai kimoja na mawindo.

After hiyo dakika kiasi ndani ya supa na ukarudi kwa ndai, ukitaka tu kuwasha dinga kitu inakushow ebu yebi tenje, kushtuka hanaku unatafuta laptop, inakua missing in action. Mara hiyo teke teke hadi kwa chogi, ukifika kwa shogi kumuuliza anakuchapia yeseye hana copy ya risto kama hiyo. Hizi ni kesi kadhaa zimekuwa zikiskika sana kwa ma parking lot mob sana za ma supa hasapa GG.

Hawa machogi kazi yao ni kuchunga hiyo ndai yako na kama umeingia supa kuboti kile unaboti but, hawa machogi ndio wamegeuka kuwa mabandi. Inasemekana saa zile chogi anapiga tero ndai yako hiyo ndio idhaa ako rada na usoro akisakanya chenye anaweza cross nayo. Venye sources zinatushow, hawa machogi huungana kimoja nao mathegi wenye wakona master key yenye wanatumia kupiga ndai yako koto.

Management ya supa inafanya kidogo sana kuhusu sarakasi kama hizi, alafu ukipeleka malalamishi kwao mabeast, complain yako inabaki kuwa jamo ya zile risto ndefu zenye zinaendelea the same kama yakoya. Hasapo ndio mudhii hukatsika na kudaisha hatawai kanyanga hiyo supa tena.

So the thing is, incase unadaisha kuingia supa na kwa kismat poa ukona co-driver ni poa ukamshow akutegee kwa ndai ukiwa unadu shopping, hasapo unaweza ponea. But mukaenda nyinyi wote tena muta dunda kwa trap ya hawa machogi.

Related Stories