Krisi iko inadi

December 28 2014 9:22pm     0 330

Photo Credit:Google   Tingua risto

Kila mvua siku ya December 25th wadhii hujibamba kwa bash ya kukumbuka kuzaliwa kwa mniaju wa Sir God. Dunia nzima hupata holiday ya kucelebrate hii day ya Krisi, na ata wasee wenye si wachristian hujinice nayo.

Njaro za kucelebrate Krisi ni kibao lakini ile imeshika vimost ni ya kuwaiana gifts. Pia kuna mambo kama; kufika chachiko, kuimba chrismas carols, kuboti miti za krisi na kuzidecorate na kudema keroma za aina zote.

Inaaminika kuna msee anatambulika kama Santa Claus ama Father Krisi, mwenye hugei watoi maprezo. Alafu mabizna humekisha ganji mwenda kupitia mapromo za kukinda stuff zenye wasee hutumia kama gifts.

Lakini hisihi ndio time fiti ya kusherekea pamoja na famo na mabeshte. Na bado wadhii wengine hupenda kutravel, sana sana kufika ocha ama kuenda places nira. Blanda bwaku lakini ni venye wasee hujisahau na kutei vimost na kubaki wamejiingisa kwa aksi mbaya.

Inafaa kukaa rada na venye unajibamba. 

Related Stories