Unadai kubaki umemarika?

January 7 2015 3:51pm     0 404

Photo Credit:thestir   Tingua risto

Vitu mob hubadilika wasee wakishamarika. Ni kama wao husahau venye walikua wanafeel matime wakikatiana. Ulovito hurushwa njei ya diro na inabaki wamekwachu divorce, alafu waniaju wanachwa wakikapitia.

Kuna njaro ya kuavoid hii noma, na italingana na both hazii na wife kama wanadai kunyeyekea. Tukianza na majamaa, kuna venye ni muhimu kutembea next na wifey. Risto za kumbetea lembe ama manyu yake, temana nayo kabisa. Ule ni totoise wa kwako, so kwama na yeseye.

 Ni poa kumtingulia mgola na ata kumshika mkono matime. Ndiwike zingine unaweza mchapa surprise na kumpeleka outing ama road trip ama ata kwa hoteli tu. Ndio acheki bado unamfikiria kama manzi yake.

Boti tuprezo ata kama si holiday. Na usingoje kukumbushwa siku za birthday na anniversaries. Alafu ile muhimu zaidi, usiwai gwaya kumchapia venye unampenda. ‘I Love You’ ndio words tatu zenye zinaweza kukutoa kwa ngori kibao.

Mambuus pia mkona wera ya kuduu kumekisha jakes zenu. Jaribu mambo nira za kuduu pamoja na hubby. Temana na risto za kununa. Badala yake, mnaweza kuwa mnacheka masaibu mshapitia, ndio ata zile fyam zikimuja, haitakuwa noma kudeal nazo.

Kuwa creative kwa lungula. Ukiamua kungoja hadi ile siku utakuwa na moods za ulovito basi itabaki umedunga hema siku mob. Kupiga hubby hugs na munju ni muhimu. Pia kusema venye unampenda ni plus. Alafu hanaku haja ya kukwamia grudges ndogo ndogo. Samehea huyo mudhii baba ya waniaju wako na muendelee na maisha.

Ile task major kwa mambuus, itakuwa kuweka mashida za kumarika zikiwa private. Risto ya kusambaza parasha za keja yako ni blanda kuruka. Endelea kukaa kama ule manzi alikatiwa hadi akaingia box na hisiyo marriage itakuwa ya vungu.

Related Stories