Mkwanja imelost kupatikana Githare Area 2!

July 2 2014 12:29pm     0 1552

Photo Credit:Go Sheng   Tingua risto

Makarao wako na wera ngumu sana, wakijaribu kusaka colleagues wao, wenye walihepa na mita sixty nine. Inasemekana ganji total kabla kugoswa, ilikua mita 82 lakini mavedi waliweza kuget 13 milli pekee. 

Wasee walipanga hiyo ugondi walikua wasita, yaani; Ap officers watatu, na Guards wa KK watatu. Walikua wanatransport hiyo cheddars kwa ndai armoured  ya KK Security, kutoka westy hadi CBK. Lakini inakaa waliona heri kujisaidia na wakapeleka ndai hadi Githare Area 2, kule waliacha hiyo mita kinde na three, yuni  na bunde zao.

Donga wa karao, Benson Kibui anadai ni wasee wanajulikana poa, kwahivyo watabambwa tu. Although kukawa na raiya wanatambua penye wamejificha, watado fiti kuchapia karao mbio.

Si mara ya fao hii risto ya mkwanja kuenda missing, wakati zinasafirishwa across jiji.  Sijui kwanini bado hawajapata solution. Na sana sana blanda iko kwa hizo Kampu za Private Security, juu wanakuwanga wameweka employees wao na njaa.  Huku mavedi pia wanalipwa mshande za mauchu, ambapo wakipata njaro ya kupenya  na hisihi ya bwerere, inabaki ishakuwa.

Related Stories