Meyhem za mamboch

November 25 2014 9:59am     0 1856

Photo Credit:Google   Tingua risto

Manze kuna venye husuyu mboch wa UG amekatsia hao wengine wote, ikikam risto za kuaminika na kuchorwa waks kwa jakes za wadhii. Juu kuna videsa nifla imekuwa ikisambaa kwa net, ikishow venye huyu Jolly Tumuhirwe amekuwa akitesa mniaju wa mdosi wake.

Kuwa ready kutoa machozi ukiyebi hisihi vida, juu hanaku msee akona akili timamu anaweza fanya kile aliduu. Ata ni bahati sana mapero wa huyo mtoi walikuwa wamefichaa kamenje kwa hao. Ingebaki mboch amemada mniaju bure tu.

Kwanza kuna support mwenda inaendea buda wa mtoi, Eric Kimanzi,  juu ya kuvunja huyu mboch, njaro ilibidi amehepa hadi karao kuzusha. Lakini mradi yake iligonga ukuta, vile yeseye alibambwa instead kwa charges za attempted murder. Na anacheki kuserve miaka kinde na kobole kwa neti.

 Sema mapero kuingiza njeve, juu wanashuku mamboch wao kama wao huduu the same. Lakini kunakuwanga na risto za side limbi, na pia mamboch wengine hukapitia ninda ya keja za madonga wao. Na hanaku ile afadhali kuliko ingine. Heri kukaa chonjo tu ndio usijipate kwa side mbaya ya law.

 

Related Stories