Ingiza mamilli pap!

June 25 2014 3:13pm     0 1820

Photo Credit:Google   Tingua risto

Imebidi hustle kuchangamka hadi haijalishi njaro msee atatumia kuomoka. Lakini chenye wasee husahau, ni eti tunafaa kukwama kwa roots zetu za kufanya mambo. Yaani kurudi kwa mashake na kuzidi kwa ukulima.

Boniface Soli ni mjamaa anatueleza venye tunahata kumek cheddars, hapo tuking’ang’ana kuishi kwa jiji na kuduu waks kwa maoffe. Boni ako miaka 55, na amekuwa waks kwa Kenya Forestry Research Institute (KEFRI), for 26 years. Anadai amekua kwa janta ya kumeesha Bamboo na amejionea venye inaigiza mkwanja kuruka.

Kwa mfano, Bamboo stick jamo inakindwa arbesa alafu kwa mwezi upate order ya kukinda pieces thao jill, mwisho wa mwezi utakafunga na mita nane safi. Alafu zibotiwa kumekisha floor, furniture, fence,cladi, makaa, vibiriti, toothpick, na ata kubrew keroro. Ata matumizi zake ni kibao zaidi.

Kuanzisha hii biz ni easy juu bamboo seedlings hukindwa rwabe tu. Alafu unaweza kuzipanda kwa greenhouse ndio uweze kupata matokeo yam bio kwa miezi sita. Heri kujisunda kwa janta kama hii coz itafanya uweze kuhit hiyo millionare mark kwa mvua moja tu.

Related Stories